Mazingira FM

Wakulima wahimizwa kuacha kuchoma mabaki ya mazao

26 March 2026, 09:31

Afisa kilimo Elton Dickson Mtani akiwa studio za radio Mazingira FM,picha na Catherine Msafiri

Afisa kilimo Elton Dickson Mtani mabaki ya mazao yana mchango mkubwa katika kuongeza rutuba ya udongo, kuhifadhi unyevu, na kupunguza mmomonyoko wa ardhi.

Na Catherine Msafiri.

Katika juhudi za kuimarisha kilimo endelevu na kulinda mazingira, afisa kilimo Elton Dickson Mtani amewasihi wakulima kubadili mtazamo wao kuhusu usimamizi wa mabaki ya mazao shambani.

Akizungumza kwenye kipindi cha Uhifadhi wa Mazingira kinachorushwa na radio Mazingira FM kwa udhamini wa Grain to Grow Foundation, Mtani amesisitiza kuwa kuchoma mabaki ya mazao ni tabia hatarishi inayochangia uharibifu wa udongo na kupotea kwa virutubisho muhimu.

Ameeleza kuwa mabaki ya mazao yana mchango mkubwa katika kuongeza rutuba ya udongo, kuhifadhi unyevu, na kupunguza mmomonyoko wa ardhi.

Mtani ametoa tahadhari kuhusu mabaki ya mazao yaliyoathiriwa na wadudu, akisisitiza umuhimu wa kuyatenganisha na kuyaondoa shambani ili kuzuia kuenea kwa magonjwa na wadudu katika mazao mapya.

Sauti ya afisa kilimo Elton Dickson Mtani

Aidha Mtani ameeleza kuwa kuna makosa mbalimbali ambayo wakulima wanayafanya wakulima ambayo yanapelekea kuondoa virutubisho shambani na inakua rahisi shamba kukabiliwa na athari.

Sauti ya afisa kilimo Elton Dickson Mtani

Kupitia kipindi hicho, wakulima wameendelea kuelimishwa juu ya mbinu bora za uhifadhi wa mazingira na namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.