Mazingira FM
Mazingira FM
25 March 2026, 18:04

wafugaji wametaja changamoto mbalimbli zinazowakabili kuwa ni Pamoja na changamoto ya malisho hasa wakati wa kiangazi, changamoto ya maji kwa ajili ya mifugo Pamoja na kukosekana kwa maafisa mifugo katika maeneo yao.
Na Adelinus Banenwa
Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Ng’wasi Kamani amepiga marufuku maafisa mifugo na uvuvi katika halmashauri zote nchini kutokaa maofisini na badala yake wakawafute wafugaji katika maeneo yao
Marufuku hiyo ameitoa leo katika kikao cha wafugaji kilichofanyika wilayani bunda kikiwakutanisha wafugaji kutoka maeneo mbalimbali nchini wengi wao kutoka mikoa ya kanda ya ziwa

Wakitoa kero zao mbele ya viongozi, wafugaji wametaja changamoto mbalimbli zinazowakabili kuwa ni Pamoja na changamoto ya malisho hasa wakati wa kiangazi, changamoto ya maji kwa ajili ya mifugo Pamoja na kukosekana kwa maafisa mifugo katika maeneo yao hali inayopelekea wafugaji hao kutibu mifugo yao kienyeji pindi inaposhambuliwa na magonjwa.


BI. RABIA ABDALLAH HAMID Mgeni rasmi katika kikao hicho katibu wa SUK anayeshughulika na masuala ya kimataifa na mjumbe wa kamati kuu ya ccm taifa amewataka wafugaji na viongozi wao kuwa na umoja na mshikamano ili kujenga chama imara na kuepuka migogoro inayoweza kusambalatisha chama hicho.
Awali akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo mwenyekiti wa wafugaji taifa Mlida Mshota amesema ameamua kuandaa mkutano huo kwa lengo la kuwakutanisha wafugaji na serikali ili waweze kufikisha kero zao na ziweze kupatiwa ufumbuzi