Mazingira FM

Akutwa amefariki chanzo chatajwa ni tembo

24 March 2026, 19:56

Baada ya jeshi la polisi kufika walifanya uchunguzi na kukabidhi mwili kwa ndugu kwa ajili ya kuendelea na taratibu za mazishi .

Na Adelinus Banenwa

Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Ngabhe Magembe Mchenya 30 mkazi wa Kijiji cha Lamadi halmashauri ya wilaya ya Busega mkoani Simuyu amekutwa amepoteza maisha kwa madai ya kukanyagwa na tembo

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu wanadai tukio hilo limetokea siku ya jumapili march 22 2026 kwa kuwa ndugu yao huyo tangu alipoondoka nyumbani alfajiri kwenda Nyatwali kumsalimia ndugu yao hakupatikana tena hadi walipomkuta amepoteza maisha eneo la Serengeti njiapanda kwenda Nyatwali.

Mariam Emmanueli mmoja wa wanafamilia amesema Ngebhe alimuaga asubuhi ya jumapili kuwa anakwenda kumuangalia ndugu yao Nyatwali lakini alipoanza kumtafuta kwa simu kujua kama amefika simu haikupokelewa mpaka jioni hali iliyomtia wasiwasi ndipo akawajulisha ndugu wengine.

Sauti ya Mariam Emmanueli mmoja wa wanafamilia

Limbu Salinja Magodi kaka wa marehemu amesema alipokea taarifa za dada yake kupotea siku ya jumapili usiku ambapo asubuhi alichukua hatua ya kutoka kwake Nyaguge kwenda Lamadi kisha kuungana na wanafamilia wengine ili kuanza kutafuta njiani hadi walipofika eneo la Nyatwali kibaoni ndipo walipoanza kuona viashilia kwamba ndugu yao atakuwa maeneo hayo.

Sauti ya Limbu Salinja Magodi kaka wa marehemu

Limbu ameongeza kuwa baada ya jeshi la polisi kufika walifanya uchunguzi na kukabidhi mwili kwa ndugu kwa ajili ya kuendelea na taratibu za mazishi .

Sauti ya Limbu Salinja Magodi kaka wa marehemu