Mazingira FM

Mahafali ya 31 Ikizu sekondari DAS atoa mwezi kwa RUWASA na TANESCO

22 March 2026, 20:25

Katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela na viongozi wengine wakikabidhi vyeti kwa wahitimu kidato cha sita Ikizu sekondari

Ikumbukwe katika mahafali hii jumla ya wanafunzi 45 wamehitimu kidato cha sita ambapo kati yao wavulana ni 26 na wasichana ni 19 ambao walianza kadato cha tano mwaka 2024.

Na Adelinus Banenwa

Katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela ametoa muda wa mwezi mmoja kwa RUWASA na TANESCO kurekebisha mazingira ya mifumo ya maji na umeme katika eneo la shule ya sekondari ya Ikizu ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Maelekezo hayo ameyatoa leo tarehe 22 March 2026 katika mahafali ya 31 ya kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo
Wakati huohuo Mtelela amemuelekeza afisa elimu sekondari Bunda DC pamoja na mkuu wa shule ya sekondari Ikizu kufika ofisini kwake March 24 ili kuona namna ya kutatua changamoto ya upungufu wa vitabu vya kiada katika shule hiyo.

Sauti ya Katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela
wahitimu kidato cha sita Ikizu sekondari

Awali wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi wahitimu kidato cha sita pamoja na kuyataja mafanikio mbalimbali waliyoyapata, pia wametaja changamoto ya upungufu wa vitabu vya kiada kutokana na kubadirishwa mtahala wa elimu pamoja na changamoto ya mikopo kwa elimu ya juu hasa kwa wanafunzi walitoka shule binafsi.

Sauti ya wahitimu kupitia risala
Mkuu wa shule ya sekondari Ikizu Mwal Bulega Petro

Naye mkuu wa shule ya sekondari Ikizu Mwal Bulega Petro kupitia taarifa ya shule, amesema shule hiyo imeendelea kufanya vizuri kwa kipindi chote katika matokeo ya kidato cha pili, cha nne na kidato cha sita
Aidha Mwal Bulega amesema shule hiyo inasomesha bure wanafunzi wanne kutoka katika kijiji cha Bukama ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jamii inayoizunguka shule hiyo ambapo shule hutoa zaidi ya milioni saba kila mwaka kwa wanafunzi hao kulipa ada na mahitaji mengine.

katika changamoto, Mwal Bulega amesema kwa sasa changamoto kubwa ni miundombinu ya maji ambayo imechakaa ukilinganisha na mahitaji, kingine ametaja suala la umeme ambapo amesema nyaya za umeme zilizopita eneo hilo ziko wazi hali inayoleta hofu kwa wanajumuiya ya Ikizu sekondari.,

Sauti ya mkuu wa shule ya sekondari Ikizu Mwal Bulega Petro
Katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela akimwagilia maji mti baada ya kuupanda ikiwa ni ishara ya utunzaji mazingira

Ikumbukwe katika mahafali hii jumla ya wanafunzi 45 wamehitimu kidato cha sita ambapo kati yao wavulana ni 26 na wasichana ni 19 ambao walianza kadato cha tano mwaka 2024.