Ujenzi wa choo kusaidia wanafunzi kutojisaidia vichani
Ujenzi wa choo kusaidia wanafunzi kutojisaidia vichani
16 March 2026, 20:47
Mtendaji Mkuu wa Vodacom kanda ya Ziwa Ezekiel Nungwi(wa nne kushoto) akikata utepe kuzindua choo chenye matundu kumi cha wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Madaraka iliyopo Kiabakari mkoani Mara, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Deocray Mtayomba(wa pili kulia) na wajumbe wa kamti ya shule wakishuhudia.
Kufutia uhaba wa matundu ya vyoo shuleni hapo,wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu walikuwa wakilazimika kujisaidia sehemu zisizo salama kwa kuogoapa kuchangamana na wenzao.
Na Mwandishi wetu
Kufuatia wanafunzi wenye mahitaji Maalum katika shule ya Msingi Madaraka wilayani Butiama Mkoani Mara kujisaidia vichakani kutokana na upungufu wa vyoo,kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom imejenga vyoo vyenye matundu 10 shuleni hapo ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Akizungumza shuleni hapo leo Machi 16,2026 wakati wa makabidhiano ya mradi huo wa ujenzi wa vyoo, Mkuu wa Shule ya Msingi Madaraka, Deocray Mtayomba amesema kufutia uhaba wa matundu ya vyoo shuleni hapo,wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu walikuwa wakilazimika kujisaidia sehemu zisizo salama kwa kuogoapa kuchangamana na wenzao.
Ameongeza kuwa mwalimu mwenye mahitaji maalum shuleni pia alikuwa akilazimika kurudi nyumbani kwaajili ya kujisaidia kutokana na changamoto hiyo ya upungufu wa vyoo.
Amesema hali hiyo kwa namna moja ama nyingine ilikuwa ikirudisha nyuma morali ya wanafunzi hao kujifunza hivyo kusababisha ushiriki wao katika masomo kuwa duni huku akisema kukamilika kwa mradi huo kutachangia ongezeko la wanafunzi wenye mahitaji maalum shuleni hapo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Madaraka Deocray Mtayomba (aliyeinama) pamoja na Mtendaji Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa ,Ezekiel Nungwi wakiwa kwneye choo kilichojengwa na Vodacom shuleni hapo.
“Shule yetu ina wanafunzi zaidi ya.1,400 ambapo 80 kati yao ni wale wenye mahitaji maalum ambapo tulikuwa na matundu mawili tu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kwahiyo wakawa wanatakiwa watumie vyoo vya kawaida na wanafunzi wengine jambo ambalo lilikuwa gumu kwao kutokana na hali zao” amesema
Amesema kwa wanafunzi wa kawaida walikuwa na upungufu wa matundu nane hivyo ujenzi huo umemaliza kabisa changamoto ya vyoo iliyokuwa ikiikabili shule hiyo hapo awali.
Mtendaji Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Ezekiel Nungwi amesema kampuni hiyo iliamua kujenga vyoo hivyo vya kisasa shuleni hapo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha elimu ikiwemo elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum.
Amesema mradi huo.uliibuliwa wakati wa mbio maalum za baiskeli maarufu kwa jina la Twende Zetu Butiaka ambapo waendesha basikeli hao walipita shuleni hapo mwaka jana na kubaini changamoto hiyo.
wanafunzi shule ya Msingi Madaraka wilayani Butiama Mkoani Mara
“Hizi mbio zinalenga kumuenzi muasisi wa taifa letu hayati Mwl Julius Nyerere na tunalenga zaidi katika kupambana na wale maadui watatu ambao ni ujinga,maradhi na afya tunataka kuhakikisha maadui hawa tunawaangamiza kwa kushirikiana na Serikali,” amesema
Amesema anaamini baada ya kukamilika kwa mradi wanafunzi hao watakuwa na mazingira bora na salama kwaajili ya kujifunza hivyo kufikia malengo yao ya kupata elimu kama ilivyokusudiwa.
Awali akizungumza Gabriel Langa kiongozi wa Mbio za Baikel twende Butiama amesema walipita katika shule hiyo na kubaini changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo katika shule hiyo.
“Lengo la mbio hizi ni kuungana na Serikali katika kuboresha huduma za elimu,afya,mazingira na michezo hivyo baada ya kuona kuna changamoto hii tuliwasilaina na kampuni ya vodacom ambao bila kusita walikubalia kutatua changamoto hii,” amesema