Mazingira FM
Mazingira FM
9 March 2026, 11:21

Duka au muuzaji wa mbegu aliyesajiliwa akikamatwa anauza mbegu ambazo siyo bora kwa mujibu wa sheria ya mbegu ya mwaka 2003 atalipa faini kati ya milioni 100 hadi milioni 500.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wakulima kutumia mbegu bora wakati wa kupanda ili kuwa na mavuno mazuri na yenye tija kwa kipato cha familia
Hayo yamesemwa March 8, 2026 kupitia kipindi cha kilimo na mifugo kinachorushwa na mazingira fm
Martine Songoma ambaye ni mkaguzi wa mbegu kutoka taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania kanda ya ziwa tosci
Martine amesema pamaoja na wito huo pia wakulima ni vema wakafika kwenye ofisi za serikali za mitaa kata na vijiji ili kujisajili katika mfumo na kupata namba ya mkulima itakayo muwezesha kununua mbegu za ruzuku.
Aidha Martine amesema kwa duka au muuzaji wa mbegu aliyesajiliwa akikamatwa anauza mbegu ambazo siyo bora kwa mujibu wa sheria ya mbegu ya mwaka 2003 atalipa faini kati ya milioni 100 hadi milioni 500.
Victor Bundala ambaye pia ni mkaguzi wa mbegu kutoka taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania kanda ya ziwa tosci amesema TOSCI wanayo majukumu mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa wazalishaji na wauzaji wa mbegu, kuthibiti ubora wa mbegu, pia kutoa elimu kwa wakulima umuhimu wa kutumia mbegu bora.