Mazingira FM
Mazingira FM
5 March 2026, 20:48

Chalamila ameipongeza TAKUKURU wilaya ya Bunda kwa usimamizi mzuri wa mradi huo, na matumizi sahihi ya fedha iliyotolewa hadi bubakiza kiasi hicho cha fedha cha shilingi million 31
Na Adelinus Banenwa
Kiasi cha shilingi milioni 363,133,211.13 zimetumika katika ujenzi wa ofisi ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wilaya ya Bunda.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo hilo lililopo katika eneo la Boma kata ya Bunda stoo wilayani Bunda, mkurugenzi wa milki TAKUKURU Emmanuel Kiabo amesema fedha zilizopokelewa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo ni shilingi milioni 394,306,302.19 na zilizotumika ni shilingi milioni 363,133,211.13 na hivyo kiasi cha fedha kilichobaki ni shilingi milioni 31,171,091.06.
Kiabo ameongeza kuwa kwa usimamizi wa TAKUKURU wilaya ya Bunda, chini ya mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Bunda wamefanikisha ujenzi huo ambao umetekelezwa kwa mfumo wa force account.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Ndugu Crispin Chalamila ameipongeza TAKUKURU wilaya ya Bunda kwa usimamizi mzuri wa mradi huo, na matumizi sahihi ya fedha iliyotolewa hadi bubakiza kiasi hicho cha fedha cha shilingi million 31
Chalamila ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dr Samia Suluhu Hasan kwa kutoa fedha za ujenzi wa ofisi kadhaa za takukuru nchini kwa ngazi za wilaya na mikoa.
Aidha mkurugenzi huyo amewataka watumishi wa TAKUKURU kuhakikisha wanaitunza miondombinu ya jengo hilo ili iweze kudumu ikiwa ni Pamoja na kutoa huduma sahihi kwa wananchi.
Awali akitoa salamu, mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Aswege Eneck Kaminyoge ameipongeza TAKUKURU wilaya ya Bunda kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa ofisi hiyo huku akiahidi kutumia mfano wa ujenzi huo kwa miradi mingine ya serikali.