Mazingira FM

Getere aonesha kutolidhishwa na kasi ya ujenzi katika baadhi ya miradi

26 February 2026, 19:05

Ameonesha kutokulidhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa zahanati ya Mahanga ambayo hadi sasa utekelezaji wake umesimama kutokana na uzembe wa watendaji

Na Mariam Mramba

Viongozi wa vijiji wametakiwa kushirikiana vizuri katika usimamizi wa fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo hali itakayosaidia kumaliza baadhi ya changamoto zinazokumba wananchi wa maeneo husika.

Hayo yamesemwa February 26, 2026 na mbunge wa jimbo la Bunda Mhe Boniphace Mwita Getere wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi pamoja na kukagua mirdi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata ya Mihingo.

moja ya miradi ambayo haijakamilika

Mbunge Getere ameonesha kutokulidhishwa na kasi ya utekelezaji wa baadhi ya miradi ikiwemo wa ujenzi wa zahamati ya mahanga ambayo hadi sasa utekelezaji wake umesimama kutokana na uzembe wa watendaji pia miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Songambele iliyopo kata ya Mgeta.

Sauti ya Boniphace Mwita Getere

Katika hatua nyingine Mbunge Getere ameahidi viti 150 na meza 150 katika shule ya sekondari ya Amali Manchimweru vyenye thamani ya shilingi milioni 9 na kutoa mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Mahanga.

Sauti ya Boniphace Mwita Getere