Mazingira FM

Ziara ya Getere mariwanda yatoa majibu waathirika wa tembo

25 February 2026, 12:26 pm

Achangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vitano vya madarasa katika shule ya msingi Sarakwa

Na Mriam Mramba

Mbunge wa jimbo la Bunda Mheshimiwa Bonphace Mwita Getere amewataka wananchi wa jimbo hilo kuwa na tabia ya  ya ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ya mendeleo na kuhoji wakati wakiona mradi umechelewa kukamilika kwa wakati

Hayo ameyasema February 24 2026 na wananchi wa kijiji cha Mariwanda  wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi pamoja na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kijijini hapo ambapo amesema wananchi wanao wajibu wakujua lini mradi unatakiwa ukamilike na sababu zinazo sababisha mradi usimalizike katika muda uliopangwa.

Mbunge huyo amempongeza mkuu wa shule ya msingi Sarakwa kwa usimamizi mzuri wa mradi wa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa pamoja na matundu sita ya vyoo mradi ambao upo hatua za mwisho za ukamilishwaji ambapo pia amechangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vitano vya madarasa katika shule ya msingi Sarakwa

Mhe mbunge pia amegusia kuhusiana na malipo ya fidia kwa wananchi ambao mashamba yao yameharibiwa na tembo pamoja na wanyama wengine waharibifu

Sauti ya Bonphace Mwita Getere

Kwa upande wao maafsa kutoka wizara ya maliasili  na utalii Dodoma Bwana Emmanuel Kasenga na Bi Frolence Tebego  waliokuwa wameambatana na mbunge wametolea ufafanuzi sula la malipo kwa wananchi ambapo wamesema hadi sasa asilimia kubwa ya waathirika wamepata sitahiki zao na ambao bado hawajapata kumechangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo jina moja kujirudia zaidi ya mara moja, namba za simu kutokuwa sahihi, pamoja na namba za account zoa kuleta changamoto wakati wakufanya malipo.

Sauti za maafsa kutoka wizara ya maliasili