Mazingira FM

Malipo ya huduma ya afya Bunda sasa kufanyika kimtandao

23 February 2026, 8:13 pm

Dr. Yusuph Stephen Wambura, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Bunda,

Dr. Wambura amesema kuwa kuanzia sasa malipo yote ya huduma za afya yatafanyika kwa kutumia namba ya malipo (Contor Number), hatua inayolenga kuimarisha uwazi

Na Thomas Masalu

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Dr. Yusuph Stephen Wambura, ametoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa malipo ya gharama za matibabu katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vilivyopo katika Bunda Mji.

Akizungumza kwenye kipindi cha Duru za habari redio Mazingira fm , Dr. Wambura amesema kuwa kuanzia sasa malipo yote ya huduma za afya yatafanyika kwa kutumia namba ya malipo (Contor Number), hatua inayolenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya sekta ya afya.

Amesisitiza wananchi kuhakikisha wanaweka fedha kwenye simu zao kabla ya kufika vituoni ili kurahisisha mchakato wa malipo na kupunguza usumbufu unaoweza kujitokeza wakati wa kupata huduma.

Kwa mujibu wa Dr. Wambura, mfumo huo unamwezesha mgonjwa kulipa moja kwa moja kupitia mitandao ya simu bila kuhusisha fedha taslimu.

Sauti ya Dr. Yusuph Stephen Wambura

Aidha, amefafanua kuwa matumizi ya Contor Number yana faida katika kubinya mianya ya rushwa, kwani yanaondoa ulazima wa kushika fedha mkononi kati ya mhudumu na mteja.

Sauti ya Dr. Yusuph Stephen Wambura