Mazingira FM
Mazingira FM
20 February 2026, 10:35 am

Amewakumbusha madereva kutoendesha wakiwa wamelewa au kwa mwendo kasi, na kuhakikisha wanaendesha wakiwa na leseni zao wakati wote.
Na Adelinus Banenwa
ASP Faustin J. Buhembere, Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Bunda, ametoa mwongozo wa kina kwa watumiaji wa barabara kuzingatia usalama wakati wote wanapokuwa barabarani.
Hayo yameelezwa leo tarehe 19 Feb 2026 kupitia kipindi cha Duru za Habari cha Radio Mazingira FM.
ASP Buhembere amesisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya barabara na kuzingatia mambo muhimu kwa watembea kwa miguu, ikiwemo kutumia vivuko au zebra crossing, na kavuka pale panapo kuwa na afisa wa polisi au mtu yeyote mwenye mamlaka.
Aidha, amesisitiza kuzingatia ishara za taa za barabarani zinazotoa mwongozo kwa magari na daraja la waenda kwa miguu.
Kuhakikisha usalama, ASP Buhembere amewataka watembea kwa miguu kutumia sehemu zinazowawezesha watumiaji wengine wa barabara kuwaona.
Kwa upande wa madereva, amekumbusha kutoendesha wakiwa wamelewa au kwa mwendo kasi, na kuhakikisha wanaendesha wakiwa na leseni zao wakati wote.
Pia amesisitiza umuhimu wa kukagua vyombo vya usafiri kabla ya kuanza safari ili kuepuka madhara kwa watumiaji wengine wa barabara, ikiwemo ajali.
Buhembere amesema haaya ni kwa mujibu wa Sheria ya Usalama Barabarani Sura No. 168, Maelejero 2023.