Mazingira FM

Wanafunzi 374 hawajaripoti shule kidato cha kwanza Bunda DC

13 February 2026, 9:10 pm

Aagiza watoto waliosalia wote wawe wameripoti shule ifikapo Feb 28 2026,

Na Adelinus Banenwa

Jumla ya wanafunzi 374 wa kidato cha kwanza 2026 halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara hawajaripoti shuleni.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Aswege Enock Kaminyoge katika kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda kilichoketi leo Feb 13 2026.

4149 sawa na asilimia 92% wamekwisha andikishwa kidato cha kwanza kati ya wanafunzi 4523 waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wilayani Bunda kwa mwaka 2026.

Amesema pamoja na kufanya vizuri katika kuhamasisha zoezi hilo pia ameagiza watoto waliosalia wote wawe waliporiti shule ifikapo Feb 28 2026,

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Aswege Enock Kaminyoge

Aidha mhe Aswege kupitia madiwani wao amezipongeza kata za Ketare kwa shule ya sekondari ya Nyaburundu na Mihingo shule ya Mwanchimeru, kwa kuhamasisha  wazazi ambapo wanafunzi wote asilimia 100 wameripoti shuleni.

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Aswege Enock Kaminyoge

Wakizungumza na Mazingira fm pembezoni mwa mkutano wa baraza baadhi ya madiwani akiwemo diwani wa ketare ambaye kata yake wanafunzi wameripoti kwa asilimia miamoja  wamesema.

Baadhi ya madiwani