Mazingira FM

Changieni damu kuokoa maisha ya mama na mtoto

12 February 2026, 11:48 am

Mratibu wa damu salama halmashauri ya mji wa Bunda,Stephano Machage akiwa studio za radio Mazingira FM, picha na Catherine Msafiri.

Mratibu wa damu salama halmashauri ya mji wa Bunda, mkoani Mara, Stephano Machage ametoa wito watu kujitokeza kuchangia damu kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Na Catherine Msafiri,

Jamii imetakiwa kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya mama wajawazito, watoto wachanga, wagonjwa wa ajali na wanaohitaji huduma za dharura, wito uliotolewa na mratibu wa damu salama halmashauri ya mji wa Bunda, mkoani Mara, Stephano Machage.

Akizungumza kwenye kipindi cha kapu letu cha radio Mazingira FM kuhusu elimu ya umuhimu wa uchangiaji damu, Machage amesema kuwa damu ni kiungo  muhimu katika uendeshaji wa mwili wa mwanadamu.

Sauti ya mratibu wa damu salama halmashauri ya mji wa Bunda,Stephano Machage

Aidha, amewashukuru na kuwaasa taasisi za elimu, mashirika ya umma na binafsi na mashirika ya dini kushiriki kikamilifu katika kampeni za uchangiaji damu ili kuhakikisha benki ya damu wilayani humo inakuwa na akiba ya kutosha wakati wote.

Sauti ya mratibu wa damu salama halmashauri ya mji wa Bunda,Stephano Machage