Mazingira FM

Wito wa upandaji miti watolewa kutunza mazingira

11 February 2026, 12:19 pm

Mkurugenzi wa BUFADESO, Baraka Kamese akiwa kwenye kikao cha uzinduzi wa mradi,Picha na Catherine Msafiri

Kamese amesema kuwa upandaji miti una mchango mkubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hasa kwa wakulima kwani shughuli zao nyingi zinategemea hali nzuri ya hewa.

Na Catherine Msafiri

Mkurugenzi wa BUFADESO, Baraka Kamese, ametoa wito kwa wananchi kupanda miti kwa ajili ya kutunza na kulinda mazingira kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.

Kamese ametoa wito huo wakati akifanya mahojiano na Radio Mazingira FM katika Kituo cha Mafunzo ya Kilimo Mseto (ATC) Bweri Musoma kwenye kikao cha uzinduzi wa mradi wa ASILI B-CC wenye lengo la kuwafundisha wakulima kuwa na uwezo wa kustaimili mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza katika mahojiano hayo, Kamese amesema kuwa upandaji miti una mchango mkubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hasa kwa wakulima kwani shughuli zao nyingi zinategemea hali nzuri ya hewa na uathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabia nchi.

Sauti ya Mkurugenzi wa BUFADESO, Baraka Kamese

Kwa upande wake, Mratibuwa wa shirika la MVIWANYA, Joel Nguvava, naye ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la upandaji miti. Nguvava amesema kuwa uhifadhi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja, na kwamba maendeleo endelevu hayawezi kupatikana bila mazingira bora.

Sauti ya Mratibuwa wa shirika la MVIWANYA, Joel Nguvava