Mazingira FM

Apoteza maisha kwa kuzama kwenye dimbwi, mwenyekiti acharuka

8 February 2026, 9:45 pm

Madaktari walithibitisha kuwa chanzo cha tukio hilo ni mtoto kunywa maji.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa wananchi kuacha tabia ya kuchimba madimbwi pamoja na mashimo ya choo kisha kubaki wazi muda mrefu ili kuepuka madhara ya watoto kudumbukia na mazalia ya mbu

Hayo yamesemwa na Mathias Maduhu mwenyekiti wa mtaa wa Nyasura C kata ya Nyasura Halmashauri ya Mji wa Bunda mkoani Mara kufuatia kifo cha mtoto Posco Joseph mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi nane aliyepoteza maisha kwa kuzama kwenye shimo la kufyatulia tofari lililokuwa limejaa maji.

Sauti ya Mathias Maduhu mwenyekiti wa mtaa wa Nyasura C

Akizungumza na Mazingira FM Mathias amesema tukio hilo limetokea tarehe 7 Feb 2026  majira ya saa tisa mchana na baada ya kupata taarifa alichukua hatua ya kufika eneo la tukio ambapo alikuta tayari mtoto akiwa ameshakimbizwa hospitali na baada ya muda mfupi alipokea taarifa kuwa mtoto huyo amepoteza maisha.

Ameongeza kuwa yeye kama mwenyekiti aliwasiliana na viongozi wa mtaa na kata  pamoja na jeshi la polisi ambapo jeshi la polisi walifika na kubeba mwili kisha kwenda kituo cha afya ambapo madaktari walithibitisha kuwa chanzo cha tukio hilo ni mtoto kunywa maji,  kisha kukabidhi mwili huo kwa ndugu ili kuendelea na taratibu za mazishi.

Sauti ya Mathias Maduhu mwenyekiti wa mtaa wa Nyasura C

Kwa upande wa Emmanuel shilla babu wa marehemu Posco Joseph amesema familia imebaki na majonzi kwa kumpoteza mtoto huyo kutokana na ilikuwa gafra sana kwa kuwa alitoka ndani kama anakwenda kucheza lakini baada ya muda ndipo walipoanza kumtafuta na baadae wanamkuta anaelea kwenye shimo la maji ambalo lipo nyumba jirani na hapo.

Sauti ya Emmanuel shilla babu wa marehemu