Mazingira FM

Ahofiwa kuliwa na mamba akiogelea ziwa victoria

6 February 2026, 7:31 pm

picha ya Mamba

Tukio hilo limetokea tangu siku ya Alhamis tarehe  5 Feb 2026 majira ya saa kumi za jioni ambapo tangu wakati huo hadi sasa jitihada za kumtafuta mtoto huyo zinaendelea.

Na Adelinus Banenwa

Mtoto mmoja aliyetambulika kwa jina la Enock Kulwa 10 mkazi wa Nansimo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda anahofiwa kupoteza maisha baada ya kushikwa na mamba wakati akiwa ziwani anaoga.

Akizungumza na Redio Mazingira Fm mwenyekiti wa Kijiji cha Kasahunga Benard Jamas Nyamega ambapo tukio hilo limetokea, amesema tukio hilo limetokea tangu siku ya Alhamis tarehe  5 Feb 2026 majira ya saa kumi za jioni ambapo tangu wakati huo hadi sasa jitihada za kumtafuta mtoto huyo zinaendelea.

Benard Jamas Nyamega

Ikumbukwe maeneo ya ukanda wa ziwa Victoria hasa yanayozunguka wilaya ya Bunda yamekuwa maeneo hatari kwa wananchi kutokana na matukio ya mamba kushika watu na kusababisha majeruhi na wakati mwingine baadhi kupoteza maisha.