Mazingira FM

90% ya wanawake hujitokeza kwenye fursa za ujasiriamali

21 January 2026, 5:23 pm

moja ya bidhaa iliyotengenezwa katika mafunzo

Mara nyingi kwenye mafunzo kama haya wanawake hufika asilimia 90 huku wanaume na vijana huwa ni asilimia 10.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa vijana na akina mama kuchangamkia fursa za kujifunza ujuzi utakaowasaidia kujikwamua kiuchumi.

Haya yamesemwa na Sarah Juma katika mafunzo ya ujasiriamali yaliyofanyika Jan 20, 2026 mjini Bunda ambapo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo vijana na akina mama kujiajiri.

Sarah ambaye ndiye muandaaji wa mafunzo hayo amesema kwa wale waliojitokeza wamejifunza mambo mbalimbali ambayo yatawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Sostenes Seth Gabriel moja ya wakufunzi
Sauti ya Sarah Juma

Sostenes Seth Gabriel moja ya wakufunzi katika mafunzo hayo amesema mafunzo hayo yamekwenda vizuri na wao kama wakufunzi nia yao ni kuona jamii kubwa ya vijana na akina mama kuchangamkia fursa za kujifunza ujuzi na ujasiriamali.

Ameongeza kuwa mara nyingi kwenye mafunzo kama haya wanawake hufika Asilimia 90 huku wanaume na vijana huwa ni asilimia 10.

Sauti ya Sostenes Seth Gabriel moja ya wakufunzi

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa semina hii ya ujasiriamali wameshukuru kwa fursa hii iliyotolewa huku wakihakikishia kutendea kazi yale mafunzo waliyoyapata.

Baadhi ya washiriki wa semina
Sauti za baadhi ya washiriki wa semina

Miongoni mwao yaliyofundishwa katika semina hii ni pamoja na utengenezaji wa Sabuni ya Maji, sabuni ya mche, shampoo, utengenezaji wa Batiki miongoni mwa masuala mengine