Mazingira FM
Mazingira FM
13 December 2025, 2:38 pm

Jamii yatakiwa kuzingatia malezi kwa watoto kuanzia ngazi ya familia badala ya wazazi kuwa bize na kazi, pia kufuata sheria ili kuepukana na ukatili wa kijinsia.
Na Adelinus Banenwa
Imeelezwa kuwa hali ya ukatili wa kutelekezwa bado ni changamoto kubwa kwa jamii ya watu wa halmashauri ya mji wa bunda ambapo kwa takwimu za mwaka huu inapindukia asilimi 70 hadi 80
Hayo yameelezwa na afisa ustawi wa jamii wa halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara Waryoba Juma Waryoba wakati akizungumza na radio Mazingira FM kuhusu siku 16 za kupinga ukatili kwa mwaka huu 2025
Waryoba amesema idara ya ustawi wa jamii ngazi ya halmashauri ya mji wa Bunda imeendelea kutoa elimu juu ya aina za ukatili, madhara ya ukati mbayo inatolewa kupitia vyombo vya habari, mikutano ya hadhara, pamoja na mashuleni elimu ambayo imeleta matokeo chanya katika kupunguza aina nyingine za ukati japo ukatili wa utelekezwaji na wa kihisia bado upo juu.
Aidha amesema mbali na mafanikio yaliyopo bado elimu inahitajika kuendelea kutolewa ambapo kwa sasa kiwango cha uelewa kwa wananchi juu ya masuala ya ukatili kinafikia asilimia 70 kutoka asilimia 40 iliyokuwepo, akitolea mfano wa tukio la hivi karibuni mtoto wa miaka 3 kubakwa na mtoto mwenzie wa miaka 13.
Waryoba ametoa wito kwa jamii kuzingatia malezi kwa watoto kuanzia ngazi ya familia badala ya wazazi kuwa bize na kazi, pia kufuata sheria ili kuepukana na ukatili wa kijinsia.