Mazingira FM

TEHAMA nguzo ya wanafunzi kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia

7 October 2025, 11:22 am

picha ya wanafunzi wa shule ya sekondari esperanto wakiwa kwenye chumba cha somo la Tehama,picha na Joseph Makori

Wanafunzi wa shule ya sekondari Esperanto waeeleza namna somo la Tehama litakavyowasaidia kukabiliana na mabadiliko na ukuaji wa ya teknolojia.

Na Catherine Msafiri

Katika dunia ya sasa inayokua kwa kasi kiteknolojia, somo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) limekuwa silaha muhimu kwa wanafunzi katika maandalizi yao ya maisha ya baadaye. Somo hili si tu kwamba linafundisha ujuzi wa matumizi ya kompyuta na mitandao, bali pia huwajengea wanafunzi uwezo wa kufikiri kisasa, kujifunza kwa kujitegemea, na kushirikiana kwa njia bunifu kupitia majukwaa ya kidijitali.

Wakizungumza na radio Mazingira FM baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Esperanto wameeleza namna somo la Tehama litakavyowasaidia kukabiliana na mabadiliko na ukuaji wa ya teknolojia kwa kuwa wataanza kujifunza kuanzia sekondari

Wameshukuru shirika la Mazingira lililofadhili mradi wa chumba cha Tehama chenye vifaa vya kisasa kama kompyuta 30,viti 31 na meza 31 na mfumo wa mtandao utakaowawezesha kujifunza kwa urahisi.

Sauti za wanafunzi

Akielezea Mradi huo mratibu wa miradi kutoka shirika la Mazingira ndugu.Simba Mramba ameeleza kuwa mradi huo umefadhiliwa na shirika hilo kwa kushirikiana na STICHTING MAZINGIRA NEDERLAND na WILDE GANZEN FOUNDATION kwaajili ya kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Tehama ili kukabiliana na mabadiliko na ukuaji wa teknolojia

Ameongeza kuwa mradi huo utakwenda kuwasaidia wanafunzi katika kukabiliana na soko la ajira

Sauti ya mratibu wa miradi kutoka shirika la Mazingira ndugu.Simba Mramba

Kwa upande wake Mwalimu wa somo la Tehama katika shule ya sekondari Esperanto Martine Elias ameeleza kuwa somo la Tehama ni pan sana na litawasaidia vijana kuapata ujuzi na uzoefu hata kuwawezesha kujiajiri na kuendana na mabadiliko na ukuaji wa Teknolojia.

Sauti ya Mwalimu wa somo la Tehama katika shule ya sekondari Esperanto Martine Elias