Mazingira FM
Mazingira FM
14 September 2025, 10:16 am

Mirumbe akiwa mgeni rasmi amewanadi wagombea wa CCM kuanzia kwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt Samia Suluhu Hassan, ubunge Ndugu Jafari Wambura Chege na madiwani wote kutoka kata 26 za jimbo la Rorya.
Na Adelinus Banenwa
Katibu wa NEC Uchumi na Fedha na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Ndugu Joshua Chacha Mirumbe amesema wananchi wanayo kila sababu ya mkumchagua mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi CCM kutokana na kazi kubwa aliyoifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo katika Sekta ya Maji ukiwemo Mradi wa maji Komuge, mradi wa maji shirati na mradi wa maji nyamagaro hadi Tarime unaogharimu zaidi ya 100 bilioni.

Ndugu Mirumbe ameyasema hayo leo Sept 13, 2025 wilayani Rorya katika viwanja vya mnada wa Nyamaguku katika uzinduzi wa kampeni katika jimbo la Rorya.

Mirumbe amesema miradi mingine ni Miundombinu inayosimamiwa na Tarura na Tanroad ujenzi lami kuruya umeanza na upembuzi yakinifu wa barabara ya Kuruya hadi Utegi, barabara ya Lami Utegi hadi Shirati, na katika upande wa Elimu Sekondari Rorya wampokea zaidi ya shilingi 600 million na katika Afya vituo vitatu vya Afya Luo imbo, Nyancha na Suba zaidi 1.2 biliion zimetumika.

Katika uzinduzi huo Mirumbe akiwa mgeni rasmi amewanadi wagombea wa CCM kuanzia kwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt Samia Suluhu Hassan, ubunge Ndugu Jafari Wambura Chege na madiwani wote kutoka kata 26 za jimbo la Rorya.