Mazingira FM
Mazingira FM
17 August 2025, 11:18 am

Viongozi na wanufaika wa msaada huo kuhakikisha vifaa hivyo vinatuzwa ili viweze kudumu kwa muda mrefu.
Na Adelinus Banenwa
Jumla ya jozi tano za jezi, viatu vya michezo jozi 12 na mipira 18 vimetolewa kwa vijana wa kata ya Namuhula iliyopo halmashauri ya wilaya ya Bunda kwa lengo la kuendeleza vijana katika sekta ya michezo.
Msaada huo wa vifaa vya michezo umetolewa na Dr Masinde Bwire ambaye ni mdau wa maendeleo ambaye pia ni katibu mkuu wa tume ya ustawi wa eneo la Ziwa Victoria

Akizungumza katika hafla ya kupokea msaada huo kwa niaba ya mkurugenzi wa halamashauri, Yustus Charles Kabwogi ambaye ni afisa michezo na utamaduni halmashauri ya wilaya ya Bunda amesema vifaa hivyo vilivyotolewa vitasaida kuongeza chachu ya michezo kwa vijana pia kuwaleta pamoja.
Ameongeza kuwa wao kama halmashauri kwa kushirikiana na wenyeviti wa vijiji vya kata ya Namuhula watakwenda kuanzisha ligi mara moja ambayo itaanzia ngazi ya vitongoji mpaka kata.
Akikabidhi msaada huo Dr Masinde amesema wao kama wadau na wazawa ameona ni vema kuja kuwatia moyo vijana lakini pia kuunga juhudi za serikali katika kuibua vipaji vya vijana kupitia michezo.

Ametoa rai kwa viongozi na wanufaika wa msaada huo kuhakikisha vifaa hivyo vinatuzwa ili viweze kudumu kwa muda mrefu.
Kwa upande wao baadhi ya wenyeviti wa vijiji vya kata ya Namuhula wamepongeza jitihada na uzalendo aliouonesha Dr Bwire kwa kuwapatia vifaa vya michezo ambapo wameomba wadau wengine kujitokeza kusaidia shughuli za maendeleo situ kwenye michezo bali pia kwenye sekta zingine .