Mazingira FM

Wazee wamchangia aliyekuwa diwani kuchukua fomu tena

27 June 2025, 9:50 am

Baadhi ya viongozi wa Baraza la wazee Nyasura wakikabidhi kiasi cha fedha kwa aliyekuwa diwani( mwenye fimbo na kikoi) kwa ajili ya kuchukulia fomu ngazi ya chama

kikao hicho siyo kampeni badala yake ni kumshukuru kiongozi huyo kwa yale aliyoyafanya”

Na Adelinus Banenwa

Baraza la wazee wa chama cha mapinduzi kata ya Nyasura Halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara wamemkabidhi fedha kiasi cha shilingi elfu hamsini aliyekuwa diwani wa kata hiyo Magigi Samweli Kiboko kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuomba kugombea udiwani wa kata hiyo.

Sauti ya Lugembe K Lugembe Mwenyekiti wa baraza la wazee chama cha mapinduzi kata ya Nyasura
Aliyekuwa diwani wa kata ya Nyasura Magigi Samweli Kiboko akitoa shukrani kwa wajumbe wa Baraza la wazee Nyasura

Hafla hiyo iliyofanyika leo June 26, 2025 katika ofisi za CCM Nyasura wamesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kiongozi huyo alifanya  kazi nzuri ambapo amefanikisha kupatikana miradi yenye thamani ya shilingi  bilion 3 katika kipindi cha miaka 5

Sauti ya katibu wa baraza la wazee CCM Nyasura Dishon Misana

Kw upande wake aliyekuwa Diwani wa kata hiyo Magigi Samweli Kiboko amesema kwa sababu ya baraka za wazee hao atachukua fomu baada ya mchakato wa chama kuanza mnamo 28 June 2025

Aliyekuwa diwani wa kata ya Nyasura Magigi Samweli Kiboko akipokea risala ya wazee
Sauti ya Magigi Samweli Kiboko

Akizungumza mwenyekiti wa baraza la wazee chama cha mapinduzi kata ya Nyasura LUGEMBE  K LUGEMBE amesema kikao hicho siyo kampeni badala yake ni kumshukuru kiongozi huyo kwa yale aliyoyafanya.