Mazingira FM
Mazingira FM
21 June 2025, 3:48 pm

Safari ya Rhobi, mafanikio yake, changamoto, na mwito wake kwa wanawake
Na. Edward Lucas
Katika jamii inayokabiliwa na mila kandamizi na uwakilishi mdogo wa wanawake katika uongozi, Diwani Rhobi Ghati kutoka Kata ya Kiore, halmashauri ya wilaya ya Tarime, mkoani Mara amesimama kama mfano wa ujasiri na mabadiliko. Kutoka kuwa ungariba hadi kuwa kiongozi anayeleta maendeleo halisi – hadithi yake ni ushahidi wa uwezo wa mwanamke anapopewa nafasi.
Makala hii maalum inayoangazia safari ya Rhobi, mafanikio yake, changamoto, na mwito wake kwa wanawake inatoa mwanga kwa wengine kushiriki kwenye uongozi.
Sikiliza makala fupi jinsi wanawake wa Mara wanavyoamka na kusimama! Ni sauti ya matumaini na mabadiliko katika mkoa wa Mara.