Mazingira FM
Mazingira FM
19 June 2025, 10:57 am

Miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilion 5.7 imetekelezwa Bunda stoo kwa miaka mitano.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa vijana kutoogopa kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi October mwaka huu.
Wito huo umetolewa na diwani wa kata ya Bunda stoo Mhe Flavian Chacha Nyamageko katika kikao cha halmashauri kuu ya CCM kata ya Bunda stoo kilichoketi tarehe 17 June 2025 kwa lengo la kupokea utekelezaji wa ilani ya chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ya 2020 ha 2025.
Flavian amebainisha kuwa kumekuwepo na kasumba ya vijana kuogopa kugombea kutokana na hofu ya kuona hawawezi lakini kupitia kielelezo chake kwa yale aliyoyafanya kwa kata ya Bunda stoo basi vijana siyo tena taifa la kesho bali vijana ni taifa la leo na la kesho.

Katika taarifa yake Diwani Flaviani amesema katika kipindi hicho kata ya Bunda stoo imepokea fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo zaidi ya shilingi bilion 5.7 ambazo zimekwenda kutekeleza miradi ya elimu , afya , maji, barabara pamoja na umeme.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM kata ya Bunda stoo wamempongeza kwa juhudi na jitihada kubwa aliyoionesha ya kuhakikisha shughuli za maendeleo zinafanyika katika kata hiyo bila wananchi kubugudhiwa kama zamani ikiwemo suala la kuchangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi iwe wa shule, zahanati miongoni mwa michango mingine.
Katika kutamatisha hotuba yake Mhe Flavian ametangaza rasmi kutetea nafasi yake ya kugombea udiwani wa kata hiyo pindi milango ya uchukuaji wa fomu za kura za maoni itakapofunguliwa juni 28 2025.