Mazingira FM

Wanafunzi Manyamanyama wahamasisha jamii kufuatilia vyombo vya habari

5 June 2025, 6:15 pm

Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Manyamanyama kwenye picha ya pamoja baada ya ziara yao Radio Mazingira fm

Jamii yatakiwa kisikiliza vyombo vya habari ili kujifunza masuala mbalimbali kama vile afya, elimu, mazingira n.k

Na Adelinus Banenwa

Wanafunzi wa kidato cha nne kutoka shule ya Sekondari ya Manyamanyama iliyopo halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara wametembelea na kituo cha Radio Mazingira Fm na kupewa elimu ya jinsi ufanyaji kazi ulivyo katika kukusanya, kuandaa hadi kurusha matangazo.

Lengo la mafunzo kupitia darasa hilo ni wao kujifunza jinsi vyombo ya habari vinavyofanya kazi kwa weledi ili kufikisha ujumbe kwenye jamii.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Manyamanyama wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Radio mazingira fm

Wanafunzi hao waliongozwa na Taro Michael Mjora kujifunza na kuzunguka kwenye vitengo mbalimbali vya kituo cha Radio Mazingira Fm ambapo wameihasa jamii kujenga tabia ya kusikiliza vyombo vya habari hususani Radio Mazingira fm ili kupata taarifa na habari mbalimbali zinazoelimisha na kuburudisha ikiwemo habari za elimu, afya, mazingira pamoja burudani na michezo.