Jiungeni NHIF kuwa na uhakika wa matibabu
11 December 2024, 6:28 pm
Lengo la NHIF ni kuwaunganisha wanachama wa NHIF katika familia moja ili kuwaka unafuu wa na uhakika wa matibabu.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya wa NHIF ili kuwa na uhakika wa huduma za matibabu pindi wanapougua.
Hayo yamesema na afisa wa NHIF mkoa wa Mara Bi. Felister Renatus Afisa mwanachama NHIF mkoa wa Mara alipozunzumza na wananchi kupitia Radio Mazingira fm katika kipindi cha Asubuhi Leo ambapo afisa huyo amesema lengo la NHIF ni kuwaunganisha wanachama wa NHIF katika familia moja ili kuwaka unafuu wa na uhakika wa matibabu.
Bi. Felister Renatus Ameongeza kuwa mfuko wa bima ya afya unavyo vifurushi mbalimbali ambavyo mwanachama anaweza kuchagua kujiunga kwa kadri anavyoweza Akitaja baadhi ya vifurushi vinavyotolewa na mfuko wa bima ya afya Bi. Felister amesema ni bima ya wanafunzi kwa shilingi 54,000, watu binafsi kuanzia kiwango cha chini shilingi 190,000/= kwa mwaka mzima pia kipo kifurushi cha wafanyakazi wa Umma na sekta binafsi miongoni mwa vifurushi vingine.
Kwa upande wake Kuhunga Msambichaka ambaye ni meneja wa NHIF ameitaka jamii kubadili mtazamo juu ya bima ya afya ambapo kumekuwepo na kasumba ya watu kuchukulia michango ya bima kama ni gharama kubwa lakini faida yake ni pale ukiumwa ambapo utahitaji matibabu ya kibingwa, NHIF inasimama matibabu kwa hicho kiasi ulichotoa kwa mwanachama.