Mazingira FM

Nance: Wenyeviti shirikianeni na watendaji kuleta maendeleo

10 December 2024, 6:16 pm

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake chama cha mapinduzi mkoa wa Mara ( UWT)  Bi  Nance Msafiri  Sesani

Kwa sasa makundi hayana tija badala yake wenyeviti wanatakiwa kuungana na viongozi wengine wakiwemo watendaji ili kuleta maendeleo katika eneo husika ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero mbalibali za wananchi kupitia mikutano ya hadhara ,kukemea vitendo vya  ukatili wa kijinsia pamoja na ukatili kwa watoto

Na Mariam Mramba

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake chama cha mapinduzi mkoa wa Mara ( UWT)  Bi  Nance Msafiri  Sesani amewaasa viongozi wa serikali za vijiji waliochaguliwa  kushirikiana na watendaji wa serikali ili kwaletea wananchi maendeleo.

Hayo ameyasema leo Dec 10 wakati akitoa semina  elekezi ya kuwajengea uwezo viongozi walioingia madarakani kutoka vijiji vitatu  vya  kata  ya  Kyanyari  wilayani Butiama mkoani Mara

Bi Nance amesema kuwa kwa sasa makundi hayana tija badala yake waungane ili walete maendeleo eneo husika ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero mbalibali za wananchi kupitia mikutano ya hadhara ,kukemea vitendo vya  ukatili wa kijinsia pamoja na ukatili kwa watoto

Sauti ya  Nance Msafiri  Sesani Mwenyekiti wa ( UWT) Mara
Baadhi ya wenyeviti na wajumbe waliohudhuria kwenye semina elekezi

Kwa upande diwani wa kata ya Kyanyari Mgingi Mhochi amesema kuwa kata ya Kyanyari imetekeleza miradi mbalimbali na kuimarisha hali ya ulinzi na usalama na kwamba  watendelea  kusimamia kwa weledi suala la mapato na mtumizi  pamoja na kuboresha miundombinu  kwenye  kata hiyo.

Sauti ya diwani wa kata ya Kyanyari Mgingi Mhochi

Nae mwenyekiti wa Chama Chamapinduzi kata ya Kyanyari Ndugu,  Alfonce Mwita amesema viongozi hao wanatakiwa kujitambua kuwa wao ni viongozi halali na wawajibike katika majukumu ya kuwatumikia wananchi na kutambua mipaka yao  ya kazi.