Ajinyonga bafuni bila kuacha ujumbe
27 October 2024, 7:30 pm
Kwa mujibu wa wanafamilia ni kuwa walipata chakula cha pamoja jana usiku bila tatizo lolote hadi pale asubuhi walipogundua baba yao amejinyonga huku bila kujua sababu hasa ya chanzo cha kujiua.
Na Adelinus Banenwa
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Mbwene Dismas Magesa (57) mkazi wa kijiji cha Bunere kata ya Chitengule halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara amekutwa amejinyonga bafuni kwake.
Akizungumza na radio Mazingira fm Afisa mtendaji wa kata ya Chitengule Neema John amesema taarifa za tukio hilo amezipata leo asubuhi Oct 27, 2024 na alipofika eneo la tukio ni kweli alikuta mwanaume huyo amejinyonga ndipo aliwapigia viongozi wengine likiwemo jeshi la polisi ,
Aidha neema aliongeza kuwa kwa mujibu wa wanafamilia ni kuwa walipata chakula cha pamoja jana usiku bila tatizo lolote hadi pale asubuhi walipogundua baba yao amejinyonga huku bila kujua sababu hasa ya chanzo cha kujiua.
Mtendaji huyo amewaasa wananchi kutojichukulia sharia mkononi ama za kujidhuru au kuwadhuru wengine pindi wanapokuwa na changamoto badala yake wawasiliana na viongozi wa maeneo husika ili waweze kuwasaidia