Nyasana wapata maji ya bomba, BUWSSA yawashukuru kwa ushirikiano
23 October 2024, 9:49 am
Wananchi wa mtaa wa nyasana wameipongeza mamlaka na serikali kwa ujumla kwa kuwakumbuka kuwafikishia huduma ya maji safi kwa kwa wametaabika kwa muda mrefu
Na Adelinus Banenwa
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA Bi Esther Giryoma akabidhi kituo cha kuchotea maji kwa wakazi wa mtaa wa Nyasana kata ya Kabasa halmashauri ya mji wa Bunda.
Akizungumza na wakazi hao Bi Esther amesema jukumu la Mamlaka ni kuhakikisha wananchi wote wanapata maji safi na salama
Aidha Bi Esther amewataka wakazi hao kujitahidi kulinda miundombinu ya maji na kukemea wale wote wenye nia ya kuhujumu pia amewasisitiza wakazi hao kulipa ankara za maji pindi wanapochota ili kuufanya mradi huo kuendelea kuwepo.
Kwa upande wao wananchi wa mtaa wa nyasana wameipongeza mamlaka na serikali kwa ujumla kwa kuwakumbuka kuwafikishia huduma ya maji safi kwa kwa wametaabika kwa muda mrefu kwa kutumia maji ya madimbwi ambayo hutumia na wanyama kama vile ng’ombe na mbuzi.
Naye mtendaji wa mtaa wa Nyasana Ferister Mbonamengi amesema kutokana na changamoto ya maji iliyokuwa inawakabili wakazi hao walilazimika kukataa ujenzi wa zahanati badala yake walihutaji sana Maji ambapo wamejitolea kuchomba mtaro wenye urefu wa kilometa sita
Bi Mbonamengi amesema bila shaka yoyote watailinda miundombinu hiyo ili iweze kudumu muda mrefu na atahakikisha wananchi wanaotumia maji wanalipa ankara zao kwa wakati.