Mazingira FM

Diwani Flaviani wa Bunda stoo awafanya UWT kuwa kijani na njano

12 September 2024, 5:10 pm

Wajumbe wa baraza la wanawake CCM Bunda stoo wakiwa kwenye sare walizopewa na diwani wa kata hiyo aliyeko katikati yao, Picha na Adelinus Banenwa

Diwani wa kata ya Bunda stoo aahidi kuwafanya viongozi wote wa CCM kwenye kata yake kupata sare za chama ifikapo 2025

Na Adelinus Banenwa

Diwani wa kata ya Bunda stoo Mhe Flavian Chacha (CCM) Nyamageko ameendelea na zoezi la kuwapatia sare za chama viongozi wa chama hicho kwa kata ya Bunda stoo.

Diwani Flavian akikabidhi sare kwa mjumbe wa baraza la UWT kata ya Bunda stoo, Picha na Adelinus Banenwa

Tarehe 11 September 2024 diwani huyo amekabidhi sare kwa viongozi wa baraza la wanawake chama cha mapinduzi UWT wa kata yake ikiwa ni muendelezo wa kugawa sare za chama kwa viongozi wa chama chake ndani ya kata

Flavian amesema malengo yake ni kuhakikisha viongozi wate wa chama cha mapinduzi kata ya Bunda stoo wanakuwa na sare za chama kuanzi viongozi wa chama mpaka jumuiya zake.

Sauti ya Diwani wa kata ya Bunda

Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya ya Bunda Bi Evodia Zumba amesema jambo analolifanya diwani huyo ni uungwana mkubwa huku akitoa rai kwa viongozi waliopewa sare hizo kuhakisha wanazivaa kwenye vikao vyote vya chama na kwa wale ambao hawatovaa zipo taratibu za kinidhamu ambazo zimeainishwa kwa utaratibu wa chama.

Sauti ya Evodia Zumba katibu UWT Bunda

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la umoja wa wanawake chama cha mapinduzi kata ya Bunda stoo wamemshukuru Mhe Diwani kwa kuwakumbuka na kuwapatia sare za chama huku wakiomba viongozi wengine kuiga mfano wake.

Sauti ya baadhi ya wajumbe wa UWT Bunda stoo