Mazingira FM

DC Naano atoa mkono wa pole familia zilizopoteza ndugu ajali ya Kyandege

27 August 2024, 5:40 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda akikabidhi kiasi cha shilingi milioni tano kwa moja ya wanafamilia ya waliopoteza maisha ajali ya gari Kyandege

Mkuu wa wilaya ya Bunda kwa niaba ya Rais Samia amekabidhi shilingi milioni tano kwa familia zilizopoteza ndugu ajali ya Kyandege Bunda na milion moja na laki nne kwa majeruhi wa ajali hiyo.

Na Naomi Lumbe

Mkuu wa wilaya Bunda  Dkt Vicent Anney Naano kwa niaba ya Rais wa jamuhuri ya muunga wa Tanzania  Dkt Samia Suluhu Hassan amewakabidhi wafiwa waliopoteza ndugu katika ajali ya Kyandege kiasi cha shilingi million tano.

Dkt  Anney, akiwa ameongozana na katibu  wa chama cha mapinduzi wilaya ya Bunda John Chonya  wametembelea  familia hizo na kutoa pole hiyo kwa niaba ya Rais kutokana na ajali ya gari iliyotokea kijiji cha kyandege tarehe 25 Agust 2024 kupelekea vifo vya ndugu zao.

Mkuu wa wilaya ya Bunda akikabidhi kiasi cha shilingi milioni moja na laki nne kwa moja ya majeruhi wa ajali ya gari Kyandege

Mbali na kiasi hicho kilichotolewa kwa wafiwa pia mkuu huyo wa wilaya amewatembelea majeruhi wa ajali hiyo wanaondelea na matibabu katika hospitali ya Bunda DDH ambapo pia kwa niaba ya Rais amekabidhi kiasi cha shilingi million moja na laki nne  1,400,000 kwa kila majeruhi, ambazo zitawasaidia katika matibabu.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Bunda

Aidha DC Naano amesema hadi kufikia leo hii takribani watu 9 wamethibitika kupoteza  maisha kutokana na ajali

Dkt Baraka James,  daktari kutoka hospitali Bunda DDH amesema hospitali hiyo ilipokea majeruhi  15 na watatu  kati  yao walipatiwa rufaa ya kwenda Bugando kutokana na majeraha  walikuwa nayo ambapo walikuwa wamevunjika mifupa akiwemo mtoto mdogo

Dkt Baraka amesema wagonjwa 12 waliendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo na baadhi wamesha ruhusiwa kurudi nyumbani. 

Sauti ya Dkt Baraka James

Nao baadhi ya wanafamilia wamemshukuru  Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania dkt  Samia Suluhu Hassani kwa kuwa na moyo wa huruma na kuwajali watanzania  na kuwagusa hata watu wenye hali ya chini na kumuomba aendelee na moyo wa upendo  na huruma.