Mazingira FM

DC Bunda azindua maktaba Esperanto sekondari

16 August 2024, 8:46 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano akikata utepe kuashiria kuzindua maktaba shule ya sekondari Esperanto, Picha na Adelinus Banenwa

Dkt Vicent Naano Mkuu wa wilaya ya Bunda amewataka wanafunzi kutumia vitabu hivyo kuongeza ujuzi na maarifa yatakayowasaidia kufanya vizuri kwenye masomo yao.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano amezindua maktaba shule ya sekondari Esperanto ikiwa ni shule ya Sita kuwa na maktaba kwa halmashauri ya wilaya ya Bunda kati ya shule 24 zilizopo.

Maktaba hiyo yenye vitabu vya kiada na ziada imefadhiliwa na shirika la Stichting Mazingira, ambapo imetajwa kuwepo kwa maktaba hiyo kutasaidia wanafunzi kujisomea.

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano akikagua baadhi ya vitabu kwenye maktaba Esperanto Secondari, Picha na Adelinus Banenwa

Katika uzinduzi huo Dkt Naano amewataka wanafunzi kutumia vitabu hivyo kuongeza ujuzi na maarifa yatakayowasaidia kufanya vizuri kwenye masomo yao.

Mbali na uzinduzi wa maktaba pia Mhe mkuu wa wilaya amezindua darasa la Kompyuta lenye kompyuta tano zitakazotumika kwa mazoezi kabla ya kuanza rasmi somo hilo mwakani ambapo kompyuta hizo zimefadhiliwa na jamii ya waongeaji wa lugha ya Kiesperanto.

sauti ya Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano

Mhe Mramba Simba Nyamkinda diwani wa kata ya Ketare amesema kupitia wafadhili na wadau mbalimbali shule hiyo imefanikiwa kupata miradi mbalimbali ikiwepo vyoo vya wanafunzi, bwalo la chakula, bweni la wanafunzi miongoni mwa miradi mingine.

Mhe Mramba Simba Nyamkinda diwani wa kata ya Ketare kushoto akiwa na baadhi ya wafadhili wa miradi shule ya Esperanto, Picha na Adelinus Banenwa

Aidha Mhe Mramba amemuhakikishia mkuu wa wilaya kuwa usimamizi wa miundombinu na miradi inayofadhiliwa inakuwa salama na  ifikapo mwakani shule hiyo itakuwa na kompyuta za kutosha kwa ajili ya kuanza rasmi somo la kompyuta.

sauti ya Mhe Mramba Simba Nyamkinda diwani wa kata ya Ketare

Mariam Amos Mwanafunzi wa  kidato cha nne  amesema uwepo wa kompyuta shuleni  hapo  utasaidia kwa kiasi kikubwa kujifunza somo la TEHAMA  ambalo tangu waanze kidato cha kwanza hawajawahi kujifunza somo hilo

Mariam Amos Mwanafunzi shule ya sekondari Esperanto, Picha na Adelinus Banenwa

Aidha Mariam amesema manufaa makubwa ya kujua kutumia kompyuta ni kuwa na fursa ya kujiajiri pindi unapomaliza shule.

sauti ya Mariam Amos Mwanafunzi shule ya sekondari Esperanto