Mazingira FM

CCM Bunda yawafunda waenezi kata kuelekea uchaguzi mitaa

9 August 2024, 7:09 pm

Mkatibu wa siasa na uenezi Bunda wametakiwa kutimiza majukumu yao na kutojihusisha na wagombea wakati viongozi kwenye nafasi hizo muda wake bado

Na Adelinus Banenwa

Katibu wa siasa na uenezi CCM Bunda Ndugu Gasper Petro Charles amewataka wananchi na wanachama wote wa chama cha mapinduzi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la mpiga kura.

Ndugu Gasper ameyasema hayo leo AUG 09 ,2024  kwenye kikao cha mafunzo kwa makatibu wa siasa na uenezi CCM Bunda kutoka kata zote 33 za wilaya ya Bunda kilichofanyika katika ukumbi wa CCM .

Sauti katibu wa siasa na uenezi CCM Bunda Ndugu Gasper Petro Charles

Mbali na wito huo Ndugu Gasper amesema leo ametoa mafunzo kwa makatibu wa uenezi kwa nia ya kuwaweka tayari kuelekea uchaguzi serikali za mitaa na kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.

Aidha amesema muda wa watu kupitapita katika maeneo ambayo bado viongozi wapo na wanaendekea na majukumu yao akitaji hiyo ni kinyume na katiba na utaratibu wa chama.

Sauti katibu wa siasa na uenezi CCM Bunda Ndugu Gasper Petro Charles

Kwa upande wao baadhi ya makatibu waenezi CCM wamesema mafunzo hayo yamesaidia kuwakumbusha majukumu yao kwa kuwa hii ni mara ya pili kupata mafunzo kama haya

Awali akizungumza na  makatibu wa siasa na uenezi CCM Bunda  Mwenyekiti wa CCM Bunda Ndugu Abraham Mayaya Magese amesema jumukumu kubwa ya viongozi hao ni kuhakikisha inafanya kazi kwa weledi

Amewataka viongozi hao kuacha makundi na kuepuka kuegemea kwa wanaotaka kugombea angali bado kwenye nafasi hizo wapo viongozi badala yake wasubiri  muda ukifika basi watajitokeza.

Sauti ya mwenyekiti wa CCM Bunda Ndugu Abraham Mayaya Magese