Mazingira FM

Naibu waziri Kundo mradi wa Kinyambwiga utoke RUWASA ikabidhiwe BUWSSA

23 July 2024, 7:01 pm

Naibu waziri wa Maji Mhe Kundo Andrew Mathew, Picha na Adelinus Banenwa

Mradi uliyodumu miaka 14 bila kufanya kazi naibu wazi wa maji Mhe Eng Kundo Mathew atoa siku kumi RUWASA kuukabidhi mradi huo BUWSSA

Na Adelinus Banenwa

Naibu waziri wa Maji Mhe Kundo Andrew Mathew ametoa siku 10 kwa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA kufanya mapitio ya mradi wa Kinyambwiga na kutoa taarifa mahitaji yake ili mradi huo uweze kufanya kazi.

Mhe naibu waziri Kundo amesema hayo katika ziara yake mjini Bunda ambapo ametembelea mradi huo wa maji uliopo mtaa wa  Kinyambwiga kata ya Guta Bunda mjini ambao zaidi ya miaka kumi umeshindwa kutoa huduma.

Mhe naibu waziri amewataka RUWASA kuupitia mradi huo kubaini changamoto zake zote kisha kuukabidhi mradi huo kwa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA kwa kuwa mradi huo upo ndani ya eneo lake la huduma.

sauti ya Naibu waziri wa Maji Mhe Kundo Andrew Mathew

Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi huo meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini Ruwasa kwa upande wa Bunda Eng Leo Respicius amesema mradi huo ulianza tangu mwaka 2014 lakini ilishindikana kufanya kazi kutokana na mashine kushindwa kusukuma maji hadi kwenye tenki pia mabomba kupasuka hali iliyosababisha mradi kusimama.