Mazingira FM

Wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kutozwa fedha hospitalini ‘donda ndugu’

13 July 2024, 9:01 am

Moja ya wananchi kata ya Kabasa mtaa wa Kung’ombe akitoa kero yake kwa mbunge kuhusu wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kutozwa fedha ya matibabu hospitali za umma, Picha na Adelinus Banenwa

Suala la wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kupata huduma bure hospitali za umma bado ni donda ndugu kutokana na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wananchi licha ya serikali kuendelea kusisitiza kuwa huduma kwa makundi hayo ni bure.

Na Adelinus Banenwa

Wananchi wa kata ya Kabasa halmashauri ya mji wa Bunda wamelalamikia suala la akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kutozwa fedha wanapokwenda kupata huduma kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na  wakati wa kujifungua kinyume na sera ya serikali.

Malalamiko hayo yametolewa kwenye mkutano wa hadhara  wa Mhe mbunge wa jimbo la Bunda mjini Robert Chacha Maboto Kwenye kata ya Kabasa  alipofika kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero zao na namna gani wanaweza kuzitatua.

Wakazi wa Kabasa wakisalimiana na Mbunge wa Bunda mjini baada ya mkutano wa hadhara mtaa wa Kung’ombe, Picha na Adelinus Banenwa

Wananchi hao wamemuomba mhe mbunge kuwasaidia kushughulikia Changamoto  hiyo kwa kuwa imekuwa kawaida kwa watumishi wa afya kuwadai fedha wananchi wanaokwenda kupata huduma kwenye huduma ambazo serikali imezitaja kuwa ni bure.

Imedaiwa na wananchi hao kuwa akina mama wajawazito wanapokwenda kujifungua hudaiwa hadi shilingi laki 100,000 na hutakiwa kununua vifaa vya kujifungulia hata kama amekuja na vifaa vyake.

sauti ya mkazi wa kabasa kuhusu wajawazito kutozwa hela
Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto kwenye mkutano wa hadhara Kung’ombe, Picha na Adelinus Banenwa

Akijibu hoja hiyo Mhe mbunge Maboto amesema jambo hilo hata bungeni limezungumzwa na halipendezi lakini pia bunge lilimuelekeza waziri wa afya kutuma walaka mwingine wa kukazia maelekezo yake ambayo pia kila mbunge apate nakala yake ili liweze kusimamiwa vizuri.

sauti ya mbunge akitoa ufafanuzi kuhusu wajawazito kutozwa fedha hospitalini