Mazingira FM

Mbunge Bulaya amjibu Msigwa,asema ni hasira za uchaguzi

4 July 2024, 7:31 am

Mbunge wa Viti maalumu CHADEMA Mhe Esther Amos Bulaya, Picha na Edward Lucas

Mhe Esther Bulaya amvaa Mchungaji Msigwa asema kilichomfanya kuhama ni hasira za kushindwa uchaguzi wa kanda ya Nyasa.

Na Adelinus Banenwa

Mbunge wa Viti maalumu CHADEMA Mhe Esther Amos Bulaya amesema Mchungaji Msigwa hakufanya vyema kuiponda CHADEMA baada ya kuhamia CCM.

Mhe Bulaya amesema sababu kubwa iliyomfanya Msigwa kuhama CHADEMA ni hasira za kushindwa kwenye uchaguzi wa kanda ya Nyasa hivyo hasira hizo zimepelekea aiponde CHADEMA.

Bulaya amesema amemsikia Msingwa akisema Chadema ni SACOSS ya mtu mmoja lakini anasahau bila Chadema yeye asingekuwa Mbunge.

Mhe Bulaya ameongeza kuwa haikatazwi mtu kuhama chama lakini je unahamaje? ametoa mfano yeye baada ya kuhama kutoka CCM hakuwahi kusema kitu kibaya chochote badala yake anawaheshimu kwa kuwa ndiyo waliomfanya afike alipo.