Mazingira FM

Mbunge Bulaya ampongeza mkurugenzi BUWSSA Giryoma

3 July 2024, 8:56 pm

Mbunge wa viti maalum Mhe Esther Bulaya kushoto na mkurugenzi wa BUWSSA Esther Giryoma kulia

Mbunge bulaya aipongeza BUWSSA kwa kazi nzuri ya usambazaji maji na usimamizi wa miradi Bunda ampongeza mkurugenzi wa BUWSSA kwa utendaji kazi

Na Adelinus Banenwa

Mbunge wa viti maalum Esther Bulaya ampongeza  mkurugenzi wa BUWSSA Bi Esther Giryoma kwa utendaji kazi anaoufanya kwenye suala la maji BUNDA

Pongezi hizo amezitoa kupitia Mazingira Fm kwenye kipindi cha Duru za habari alipofika kuzungumza na wakazi wa mkoa wa Mara mara baada ya kutoka kwenye Bunge la Bajeti la mwaka wa fedha 2024 na 2025.

Mhe Esther Bulaya amesema mkurugenzi huyo anajitahidi sana katika kusimamia sekta ya maji na usafi wa mazingira Bunda hasa kwenye usimamizi wa miradi ya maji inayotekelezwa.

Aidha amesema ingawa yapo malalamiko mengi kutoka kwa wateja kuhusu bili za maji na gharama zake.

Sauti ya Mhe Esther Bulaya

Amesema ingawa kazi nzuri imefanyika bado ipo changamoto kubwa ya upotevu wa maji mjini bunda ambapo kwa mamlaka za maji Bunda ni ya tatu kwa upotevu wa maji huku akitaja baadhi ya miradi inayotekelezwa ikiwa ni pamoja na mradi wa misisi Zanzibar, Balili – Kunzugu. ambapo utekelezaji wake unaendelea.

Amesema wao kama wawakilishi wa wananchi wanalo jukumu kubwa la kuwasaidia wananchi ambao ndiyo kipaumbele chao.

Bulaya amesema kila kiongozi anahitajika kuacha alama pindi anapotoka kwenye nafasi yake na ili kuleta maendeleo nilazima kuweka itikadi za vyama pembeni na kuweka maslahi ya wananchi mbele.