Mazingira FM

“Usitoe namba yako ya siri ya tigo pesa kwa yeyote”

3 July 2024, 8:10 pm

Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja tigo mkoa wa Mara Ndugu Athanas  Peter, Picha na Adelinus Banenwa.

Usitoe namba yako ya siri ya tigo pesa kwa mtu yeyote hata kwa vijana wetu wa tigo hata kama ana tisheti au kitambulisho“.

Na Adelinus Banenwa

Tahadhari imetolewa kwa wananchi kutokutoa namba zao za siri za mitandao ya simu kwa vijana wanaopita kusajili namba za simu mtaani ili kuepuka kuibiwa fedha zao.

Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja tigo mkoa wa Mara Ndugu Athanas  Peter wakati akizungumza na Mazingira Fm kupitia kipindi cha asubuhi leo July 3, 2024 ambapo alifika kufafanua program mpya ya tigo inayojulikana kama Sako kwa Bako.

Sauti ya Athanas  Peter
Meneja wa tigo mkoa wa Mara ndugu Rogiez Mbio

Kwa upande wake meneja wa tigo mkoa wa Mara ndugu Rogiez Mbio amesema kwa kuwajali wateja kampuni ya tigo tayari imehakikisha kila sehemu yenye changamoto ya mawasiliano wanasimika minala ambayo inasaidia kutatua changamoto hizo ndani ya mkoa wa mara

Mbio amesema kuwa  ndani ya mwezi huu wa saba minara mitatu itazinduliwa ndani ya mkoa wa Mara mabayo ni mnara uliopo wilaya ya Serengeti katika kijiji cha Nyambureti, Nyasurura, pamoja na Machochwe.

Sauti ya Rogiez Mbio