Mazingira FM

Kukosa choo bora mjini faini laki 5 na kifungo miezi mitatu

3 July 2024, 2:34 pm

Afisa afya kutoka halmashauri ya mji wa Bunda  Wilfred Morrison Gunje, Picha na Adelinus Banenwa

Usipokuwa na choo bora na unaishi mjini basi faini yake ni laki tano au kwenda jela miezi mitatu au vyote kwa pamoja

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa wakazi wa waoishi maeneo yote ya mjini na karibu na vyanzo vya maji kuzingatia usafi wa mazingira kwa mujibu wa sheria za nchi zinavyotaka.

Akizungumza na Mazingira FM afisa afya kutoka halmashauri ya mji wa Bunda  Wilfred Morrison Gunje amesema ni wajibu wa kila mwananchi na mkazi wa Mjini Bunda kuhakikisha anafuata sheria za mazingira ili kusaidia kuepusha magonjwa ya mlipuko na uchafuzi hovyo wa mazingira.

Gunje amesema sheria ya mazingira inataja ni marufuku kwa wakazi wa mijini kukosa vyoo bora kwenye  nyumba zao pamoja na maeneo ya umma.

Sauti ya Wilfred Morsoni Gunje

Amesema kukosa choo bora kunaweza kupelekea watu kujisaidia hovyo hivyo kusababisha magonjwa ya milipuko ambapo pia ni kosa kwa mujibu wa sheria mama za jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambayo inajulikana kama shria ya afya  namba 1 ya mwaka 2009(PUBLIC HEALTH ACT (1) 2009) na sheria ndogo za halmashauri ya mji wa Bunda.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa sheria hizo ukibainika mazingira yako iwe ni ya biashara au nyumbani au kukosa choo basi zipo adhabu na faini ambazo zimeainishwa kwa mujibu wa sheria hizo ikiwepo kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo kisichozidi miezi mitatu au faini isiyozidi laki tano au vyote kwa pamoja

Sauti ya Wilfred Morsoni Gunje