Mazingira FM

Siku 7 zatolewa Bunda TC na Bunda DC kugawana mali na madeni

27 June 2024, 12:47 pm

Mkuu wa mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi. Picha na Adelinus Banenwa

Siku saba zatolewa kwa halamshauri za Bunda kugawana mali na madeni.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi ametoa siku saba 7 kwa Halmashauri ya wilaya ya Bunda na halmashauri ya mji wa Bunda kugawana mali na madeni ambayo yalikuwepo kipindi wanatengana kimamlaka.

Kanal Mtambi amesema utekelezaji huo unaanza tarehe 27 Juni 2024.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi

Maagizo hayo ameyatoa Juni 26, 2024 katika kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda cha kujadili hoja za ukaguzi za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG kwa mwaka 2022 na 2023.