Mazingira FM

Walimu watakiwa kutojiona wanyonge serikali inatambua mchango wao

21 June 2024, 2:14 pm

Naibu katibu mkuu wizara ya Rais TAMISEMI anayeshughurikia upande wa elimu.  Dkt Charles Msonde, Picha na Adelinus Banenwa.

Walimu msijione wanyonge kazi yenu serikali inaitambua hivyo timizeni wajibu wenu pia fanyeni kazi acheni mazoea hakuna mwanafunzi mjinga wala dhana ya shule ya serkali haifaulishi.

Na Adelinus Banenwa

Naibu katibu mkuu wizara ya Rais TAMISEMI anayeshughurikia upande wa elimu  Dkt Charles Msonde amewataka walimu kutojiona wanyonge kwa kuwa ni watu muhimu katika jamii.

Dkt Msonde amesema hayo katika kikao kazi na walimu wote wa halmashauri ya wilaya ya Bunda alipokutana nao leo Juni 20 2024 chuo cha ualimu Bunda akiwa ameianz ziara yake mkoani Mara.

Amesema tangu enzi za kupatikana uhuru hadi kipindi cha awamu ya sita serikali zimeendela kuutambua mchango wa walimu katika taifa.

Baadhi ya walimu kutoka wilaya ya Bunda walioudhulia kikao cha kupokea maelekezo kutoka wizara ya OR – TAMISEMI

Amesema mwalimu Julias K Nyerere alizitambua nafasi mbili za mwalimu katika jamii ambapo ni kuwa mlezi, na kutoa ujuzi kwa wanafunzi na jamii katika taifa.

Sauti ya Dkt Charles Msonde,

Aidha dkt Charles Msonde amesema changamoto kubwa ni walimu kutokumbukwa na wanafunzi wao kwa kazi wanayoifanya.

Baadhi ya walimu kutoka wilaya ya Bunda walioudhulia kikao cha kupokea maelekezo kutoka wizara ya OR – TAMISEMI

Katika hatua nyingine Dkt msonde amewataka walimu kutimiza majukumu yao kwa kuwa wanafanya kazi nzuri ya kutoa ujuzi na pindi mwanafunzi anapofeli basi moja kwa moja mwalimu ndiye anayekuwa amefeli.