Mazingira FM

“Serikali isimamie program ya mazoezi kwa wazee”

14 June 2024, 4:47 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano katika akiwa na baadhi ya viongozi wa baraza la wazee taifa, Picha na Adelinus Banenwa

Utu,usalama na ustawi ni nyenzo ya kutokomeza ukatili dhidi ya wazee.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa serikali kusimamia program za mazoezi kwa wazee ili waweze kuwa na afya bora.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wazee kwenye siku ya kwanza katika siku tatu za maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee ambayo yanafanyika viwanja vya shule ya msingi miembeni mjini Bunda.

Wazee wakishiriki mchezo wa kuvuta kamba, Picha na Adelinus Banenwa

Wazee hao wamesema mara nyingi inaonekana wazee wanashambuliwa na magonjwa nyemelezi kutokana kukosa mazoezi ya mara kwa mara jambo linalopelekea upweke na msongo wa mawazo kwa wazee.

Wazee walioshiriki mchezo wa mpira wa miguu wakiwa kwenye picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano, Picha na Adelinus Banenwa

Katika siku ya kwanza ya maadhimisho haya wazee wamepata fursa ya kupima afya zao bure pia wameshiriki michezo mbalimbali ikiwepo kuvuta kamba, mpira wa miguu, kukimbiza kuku na kukimbia kwenye magunia.

Wazee wakiendelea na mchezo wa mpira wa miguu, Picha na Adelinus Banenwa

Ikumbukwe maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee kitaifa yanafanyika tarehe 15 June ambapo kwa mwaka huu yanafanyika wilayani Bunda mkoani Mara ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu Mhe Dr. Doroth Gwajima.