Mazingira FM

Halmashauri ya Bunda DC wapongezwa utekelezaji wa miradi

29 May 2024, 6:15 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano, Picha na Adelinus Banenwa

halmashauri ya wilaya ya bunda yapewa kongole na mkuu wa wilaya kuhusu kusanyaji wa mapato

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Bunda kwa utekelezaji wa miradi kwa ufanisi.

Mhe Naano ameyasema hayo kwenye kikao cha robo ya tatu cha  baraza la madiwani kwenye halmashauri hiyo kilichofanyika May 27, 2024.

Dc Naano amesema kwa sasa miradi ya halmashauri inafanyika vizuri na inamuelekeo mzuri wa usimamizi tofauti na zamani ilivyokuwa halmashauri ya wilaya kuwa sifa ya miradi isiyokamilika.

Moja ya madiwani akitoa hoja yake kwenye mkutano wa baraza la madiwani

Pia amesema halmashauri ina muelekeo mzuri wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ambapo hadi sasa halmashauri imeshakusanya zaidi ya asilimia 80% ya malengo ikiwa bado miezi miwili mwaka wa fedha kukamilika tofauti na zamani ambapo  asilimia kama hiyo ilikuwa ndicho kiwango cha mwisho cha halmashauri mwisho wa mwaka.

Aidha ameitaka halmashauri kupitia baraza kuhakikisha zahanati ya kyandege inakamilika kwa wakati ili kufikia tarehe 31 July mwaka huu iwe imeanza kutoa huduma.

sauti ya Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano