Mazingira FM

Changamoto ya maji, barabara na umeme kupatiwa ufumbuzi Bunda stoo

24 May 2024, 10:43 am

Mhe Flavian Chacha Nyamageko diwani kata ya Bunda stoo

ukosefu wa maji, umeme na barabara kwenye eneo la kisiwani mtaa wa Idara ya maji na Kilimani kupatiwa ufumbuzi hivi karibuni.

Na Adelinus Banenwa

Mhe Flavian Chacha Nyamageko diwani kata ya Bunda stoo amefanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi kwenye mtaa wa Kilimani uliopo kata ya Bunda stoo ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara yake kwenye mitaa yake.

Wananchi wa kata ya Bunda stoo kwenye mkutano wa diwani kusikiliza kero za wananchi

Katika ziara hiyo wananchi wamezitaja changamoto mbalimbali ikiwemo maji, barabara, umeme, upimaji wa viwanja miongoni mwa changamoto zingine.

sauti ya wananchi kero za maeneo yao

Katika majibu yake mhe diwani Flavia Chacha amesema suala la barabara lilichelewa kutokana na mvua zilizokuwa zinanyesha lakini kutokana na mvua kuisha muda wowote barabara hizo zitaanza kulimwa kwa kiwango cha changalawe na tayari mkandarasi yupo.

Mhe Flavian Chacha Nyamageko diwani kata ya Bunda stoo

Kwenye changamoto ya maji Mhe Flavian amesema tayari amewasiliana na mkurugenzi wa maji Bunda na ndani ya siku chache huduma itakuwa inawafikia.

sauti ya diwani kuhusu yaliyojili kwenye mkutano