Mazingira FM

Onyo! watumishi wasiyotoa ushirikiano kwa waandishi: RC Mtambi

19 May 2024, 1:04 pm

Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evance Mtambi akiwa na Kaimu Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mara Raphael Okelo, Picha na Adelinus Banenwa

“Kama wewe ni mtumishi wa serikali mkoa wa Mara na hutaki kutoa habari kwa waandishi mimi nakuona ni msaliti”

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evance Mtambi ametoa onyo kwa watumishi wa serikali mkoani Mara wasiotoa ushirikiano  kwa waandishi wa habari kuwa wanamhujumu Rais Samia Suluhu.

kanali mtambi ameyasema hayo wakati akifunga Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari mkoani Mara yaliyoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa Mara(MRPC) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali

RC Mtambi amesema kwa mtumishi wa serikali kukataa kutoa  taarifa kwa waandishi angali miradi iliyotekelezwa na serikali inaonekana basi yeye anamuona kama msaliti. 

Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evance Mtambi mwenye tai kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya wilaya ya Bunda waliosimama nyuma ya meza kuu.

Amesema, serikali ya awamu ya 6 chini ya .Rais Samia imefanya mambo mengi makubwa ya maendeleo ambayo yanatakiwa kufahamika kwa wananchi,anashangazwa na wanaoshindwa kutoa taarifa.

sauti ya Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evance Mtambi
Kaimu Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mara Raphael Okelo, Picha na Adelinus Banenwa

Awali akisoma taarifa mbele ya mkuu wa mkoa  Kaimu Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mara Raphael Okelo amesema mkoa wa Mara una Waandishi wa Habari zaidi ya 60 na wamekuwa wakitekeleza majukumu yao licha ya changamoto mbalimbali

Amesema wanamshukuru mkuu wa mkoa na ofisi yake kwa ushirikiano wanaopata Waandishi wa Habari na kuziomba ofisi nyingine ziige mfano huo.