Mwl. James: waibueni watoto wenye mahitaji maalumu fulsa zipo
11 July 2023, 10:54 am
Wananchi watakiwa kutowaficha watoto wenye mahitaji maalumu kwa kuwa sasa serikali inatoa nafasi kubwa kwao katika sekta ya elimu
Na Adelinus Banenwa
Wito umetokewa kwa jamii wazazi na walezi mjini Bunda kuwaibua watoto wenye mahitaji maalumu Ili waweze kupata elimu itakayowasaidia katika kutimiza ndoto zao.
Hayo yamesemwa na James Masegwe Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mazoezi wakati akizungumza na Mazingira Fm iliyofika shuleni hapo kuzungumza na Mwalimu huyo juu ya Changamoto zinazowakumba watoto wenye mahitaji maalumu.
Shule ya Mazoezi ni miongoni mwa shule za ziliyopo katika halmashauri ya mji wa Bunda inayowahudumia watoto wenye mahitaji maalumu.
Mwl. James Masegwe amesema hadi hivi sasa shuleni hiyo ina jumla ya watoto wenye mahitaji maalumu wapatao 86 ikiwa wavulana ni 54 na wasichana 32.
Aidha Mwl James amesema serikali imeleta mradi wa ujenzi wa Bweni kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu itakayochukua wanafunzi 80 litakaloghalimu shiling milioni 156 ambapokwa sasa bweni lipo katika hatua ya kuezeka.
Amesema changamoto kubwa kwa sasa ni mtazamo hasi kwa jamii kuweza kuwaibua watoto wenye mahitaji maalumu ili waweze kupata haki yao ya kupata elimu.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Nyasura Magigi Kiboko amewataka wakazi wa kata hiyo kuipenda miradi inayoletwa kweny kata hiyo na kukubali kuchangia pale inapoitajika.