Dkt Tinuga; Serikali inatambua mchango mkubwa wa wauguzi
24 May 2021, 11:59 am
Maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani kwa mkoa wa Mara imefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambapo mgeni Rasmi alikuwa mganga mkuu wa mkoa wa Mara DKT FROLIAN TINUGA kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa
Katika kujibu risala ya wauguzi Dkt Tinuga amewakumbusha baadhi ya wauguzi kuhakikisha wanafanyia kazi changamoto ambazo mara nyingi wagonjwa huwalalamikia pale wanapopata huduma licha ya kwamba Wauguzi hao wanatoa mchango mkubwa sana katika idara ya Afya
Awali mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mwl Amosi Kusaja aliwapongeza wauguzi kwa kuwa mstari wa mbele katika kutetea maisha ya watu licha ya changamoto nyingi wanazokabiliana nazo
Naye mkuu wa wilaya ya Bunda kama mgeni wa heshima katika maadhimisho hayo amesema anatambua mchango wa wauguzi hasa kwa kutokuwa wabaguzi kwa wagonjwa pasipokujali hali ya mgonjwa tofauti na fani zingine
Awali akisoma risala mwenyekiti wa wauguzi Mkoa wa Mara Ngeleja Lupeleleja amesema Wauguzi wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutopandishwa vyeo, mishahara pamoja na idadi ndogo ya wauguzi ikilinganisha na mahitaji jambo linalopelekea wauguzi kuhudumia wagonjwa wengi zaidi kuliko inavyoshauriwa.