Milion 80 kujenga madarasa manne kata ya Bunda stoo
27 April 2021, 6:05 am
Diwani wa kata ya bunda stoo Flaviani Chacha amewapongeza wadau wa maendeleo kwa kuendelea kujitolea katika kuisaidia serikali kutatua kero za wananchi
Akizungumza na Redio Mazingira Fm April ,22/ 2021 Flavian amesema amepokea shilingi milion 80 kutoka kwa wadau wa maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne katika shule mbili zilizopo kata ya Bunda stoo
Katika hatua nyingine ameipongeza serikali kupitia wizara ya tamisemi kuhusu madiwani kuijadili TARURA kwa maana imekuwa changamoto sana hasa katika kushughurikia barabara za ndani
Vilevile amezungumzia upande wa nyongeza ya posho kwa madiwani Flavian amesema serikali ni lazima ilitazame kwa kuwa inaweza kuchangia madiwani kushindwa kutoa hoja kwa mkurugenzi