Mazingira FM

Recent posts

21 June 2023, 10:47 am

TRA: Wafanyabiashara lipeni kodi msisubiri siku ya mwisho kuna faini

Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa Mara, Geofrey Comoro amewaasa wafanyabiashara wasisubiri siku ya mwisho kufanya malipo ya kodi ya mapato bali wafanye mapema ili kuepuka faini na usumbufu usio wa lazima. Comoro ameyasema…

21 June 2023, 10:40 am

CHADEMA: Ugumu wa maisha kwa vijana chanzo cha kucheza kamari, kubeti

Chama cha Demokrasia na Maendeleo  CHADEMA kimefanya mkutano katika kata ya Bunda Stoo halmashauri ya mji wa Bunda huku wakigusia mambo mbalimbali likiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana  na ugumu wa maisha. Katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya…

9 June 2023, 8:48 am

Anusurika kifo baada ya kuchomwa kisu tumboni

Janeth Samweli (28) mkazi wa mtaa wa Kabarimu kata ya Kabarimu halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara amenusurika kifo baada ya kuchomwa kisu na anayetajwa kuwa na mume wake tumboni kisha mwanaume huyo kutokomea kusikojulikana. Wakizungumza na Mazingira Fm…

9 June 2023, 7:43 am

Zitto: Bei ya pamba iendane na gharama za uzalishaji

Kufuatia kilio cha wakulima wa zao la pamba nchini hususani katika bei ya pamba, chama cha ACT-Wazalendo kimewaelekeza wachambuzi wake kuangalia iwapo bei hiyo inaweza kusaidia mkulima kurejesha gharama zake alizozitumia katika kilimo. Hayo yamebainishwa na kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto…

7 June 2023, 2:12 pm

Zito Kabwe kuunguruma Musoma

Chama cha ACT Wazalendo kesho tarehe 8 Juni 2023 kitafanya mkutano mkubwa wa siasa katika viwanja vya shule ya msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara. Hii ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake tangu ilivyozindua mikutano hiyo mwezi Februari 2023…

7 June 2023, 12:32 pm

Bunda: Wakazi kata Manyamanyama wanufaika mabomba ya maji

Diwani wa kata ya Manyamanyama Mhe Mathayo Machilu amekabidhi mabomba ya maji yenye urefu wa mita 950 eneo la kisiwani Mtaa wa Mbugani kata ya Manyamanyama. Akizungumza katika kikao hicho cha kukabidhi mabomba hayo Mhe Machilu amesema kama alivyoahidi katika…