Nance: Wenyeviti shirikianeni na watendaji kuleta maendeleo
10 December 2024, 6:16 pm
Kwa sasa makundi hayana tija badala yake wenyeviti wanatakiwa kuungana na viongozi wengine wakiwemo watendaji ili kuleta maendeleo katika eneo husika ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero mbalibali za wananchi kupitia mikutano ya hadhara ,kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na ukatili kwa watoto
Na Mariam Mramba
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake chama cha mapinduzi mkoa wa Mara ( UWT) Bi Nance Msafiri Sesani amewaasa viongozi wa serikali za vijiji waliochaguliwa kushirikiana na watendaji wa serikali ili kwaletea wananchi maendeleo.
Hayo ameyasema leo Dec 10 wakati akitoa semina elekezi ya kuwajengea uwezo viongozi walioingia madarakani kutoka vijiji vitatu vya kata ya Kyanyari wilayani Butiama mkoani Mara
Bi Nance amesema kuwa kwa sasa makundi hayana tija badala yake waungane ili walete maendeleo eneo husika ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero mbalibali za wananchi kupitia mikutano ya hadhara ,kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na ukatili kwa watoto
Kwa upande diwani wa kata ya Kyanyari Mgingi Mhochi amesema kuwa kata ya Kyanyari imetekeleza miradi mbalimbali na kuimarisha hali ya ulinzi na usalama na kwamba watendelea kusimamia kwa weledi suala la mapato na mtumizi pamoja na kuboresha miundombinu kwenye kata hiyo.
Nae mwenyekiti wa Chama Chamapinduzi kata ya Kyanyari Ndugu, Alfonce Mwita amesema viongozi hao wanatakiwa kujitambua kuwa wao ni viongozi halali na wawajibike katika majukumu ya kuwatumikia wananchi na kutambua mipaka yao ya kazi.